Liverpool itakuwa nyumbani Anfield ikisaka kurekebisha matokeo dhidi ya Paris Saint-Germain katika mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kupoteza 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Paris.
Kikosi cha Arne Slot kinahitaji ushindi wa kishindo ili kusonga mbele, huku presha kubwa ikiwa kwa wachezaji wake wakongwe kama Mohamed Salah na Andrew Robertson ambao huenda wakacheza mechi muhimu ya Ulaya katika klabu hiyo.
Mashabiki wa Anfield wanatarajiwa kuipa Liverpool nguvu kubwa, huku historia ikionesha mara nyingi klabu hiyo hucheza vizuri katika mazingira ya nyumbani kwenye mechi za Ulaya.
CHANZO: TRT Afrika














