Siasa Afrika Ulimwengu

DRC kuwapokea wahamiaji kutoka Marekani kwa mara ya kwanza

Hatua hii ni sehemu ya makubaliano mapya ya uhamiaji kati ya Marekani na DRC.

Newstimehub

Newstimehub

15 Aprili, 2026

622

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inatarajiwa kuwapokea zaidi ya wahamiaji 30 kutoka Marekani wiki hii, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano mapya ya uhamiaji kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa vyanzo, idadi ya wahamiaji inaweza kufikia kati ya 37 hadi 45, huku wengi wao wakitoka Amerika ya Kati na Kusini, na si raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hatua hii inaifanya DRC kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zinazokubali kupokea wahamiaji kutoka Marekani.

CHANZO: TRT Afrika