Mohamed Salah amezua sintofahamu baada ya kulalamika kuwa Liverpool imemsaliti kwa kumweka benchi kwa mara ya tatu mfululizo, jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi. Mshambuliaji huyo, aliyekataa ofa kubwa ya Saudi Arabia ili kubaki Anfield, amesema anahisi “kudhalilishwa” na kutendewa kama “mchezaji wa daraja la tatu.”
Vyombo vya habari Uingereza vimekosoa kauli zake na kubashiri kuwa huenda tayari ameshacheza mechi yake ya mwisho na Liverpool. Licha ya msimu uliopita kung’ara kwa mabao 34 na pasi 23, mustakabali wa Salah sasa umejaa utata.
CHANZO: TRT Afrika














