Majengo mawili ya makazi katika eneo la Al-Massira, Fes kaskazini mwa Morocco, yameporomoka na kusababisha vifo vya watu 22 na kujeruhi 16. Vikosi vya uokoaji viliendelea kuwatafuta manusura, huku wakazi wa karibu wakihamishwa kwa tahadhari. Waendesha mashitaka wameamuru uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio, ambacho hadi sasa hakijajulikana.
CHANZO: TRT Afrika














