Waziri wa Maji wa Morocco, Nizar Baraka, ametangaza kuwa ukame uliodumu kwa miaka saba nchini humo umefikia kikomo kufuatia mvua kubwa za msimu wa baridi.
Baraka aliwaambia wabunge kwamba kiwango cha mvua kimeongezeka kwa 95% ikilinganishwa na mwaka uliopita na ni 17% zaidi ya wastani wa msimu. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa mabwawa yamejaa kwa 46%, na hifadhi za maji zimeimarika kwa kiasi kikubwa.
Mvua hizo zimeleta nafuu kubwa kwa sekta ya kilimo, ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto za uhaba wa maji kwa muda mrefu.
CHANZO: TRT Afrika














