Afrika

Makamu wa Rais Nchimbi atoa wito wa mshikamano katika maadhimisho ya CCM

Maadhimisho ya miaka 49 ya CCM yamefanyika Februari 5, 2026 katika Wilaya ya Chemba, Dodoma.

Newstimehub

Newstimehub

5 Februari, 2026

402

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amehudhuria maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika Februari 5, 2026 katika Wilaya ya Chemba, Dodoma.

Katika hotuba yake, Dkt. Nchimbi aliwataka wanachama wa CCM kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa kuhakikisha chama kinaendelea kuwa cha Watanzania wote na kimbilio la wananchi. Alisisitiza kuwa kila mwanachama na kiongozi anatakiwa kutafakari matendo yake na mchango wake katika kuimarisha maendeleo, mshikamano wa chama na umoja wa Taifa.

Aidha, alieleza kuwa chama kinapoelekea katika uchaguzi wa ndani kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa mwaka 2027, ni muhimu wanachama kujiandaa mapema kwa kuzingatia misingi ya kulinda maadili ya chama, kudumisha mshikamano, kuendeleza amani na utulivu, na kutambua kuwa uongozi ni dhamana ya kuwatumikia wananchi.

CHANZO: TRT Afrika