Uturuki imelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea katika Jimbo la Kwara, Nigeria, na kusababisha vifo vya takribani watu 170. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilieleza huzuni kubwa kutokana na tukio hilo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na wananchi wa Nigeria.
Wizara hiyo imethibitisha mshikamano wa Uturuki na Nigeria na kusisitiza kuwa itaendelea kuunga mkono juhudi za nchi hiyo katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Shambulio hilo lilifanywa na makundi yenye silaha siku ya Jumanne, na limeongeza hofu ya usalama katika Jimbo la Kwara, hususan maeneo ya vijijini karibu na misitu. Katika miezi ya hivi karibuni, jimbo hilo limekumbwa na ongezeko la ujambazi, utekaji nyara, na makundi yenye silaha yanayotoroka operesheni za kijeshi katika majimbo jirani ya kaskazini-magharibi na kaskazini ya kati.
CHANZO: TRT Afrika














