Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha mpango mpya wa msaada wa kifedha kwa Liberia wenye thamani ya takribani dola milioni 266, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi nchini humo.
Kati ya fedha hizo, dola milioni 26.49 zitatolewa mara moja ili kusaidia juhudi za serikali katika kuimarisha uthabiti wa uchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mpango huo wa miezi 21 unalenga pia kusaidia Liberia katika kudhibiti deni la taifa, kuimarisha mfumo wa kifedha na kuboresha utawala bora.
IMF imesema uchumi wa Liberia umeonyesha ukuaji wa asilimia 5.1 mwaka 2025, unaochochewa zaidi na shughuli za uchimbaji madini.
CHANZO: TRT Afrika














