Ulimwengu

Trump azindua tovuti ya dawa nafuu, TrumpRx

“Kuanzia jioni ya leo, dawa nyingi zinazotumika mara kwa mara zitapatikana kwa punguzo kubwa kwa watumiaji wote.” — Donald Trump

Newstimehub

Newstimehub

6 Februari, 2026

407

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuzindua tovuti mpya iitwayo TrumpRx, inayowezesha wananchi kupata dawa za kutumia kwa maagizo ya daktari kwa bei nafuu. Akizungumza Ikulu ya White House, Trump alisema kuwa dawa nyingi zinazotumika mara kwa mara sasa zitapatikana kwa punguzo kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makampuni ya dawa Eli Lilly na Novo Nordisk yamekubali kutoa punguzo kubwa kwa dawa za kupunguza uzito zinazojulikana kama anti-GLP-1. Bei ya Ozempic kutoka Novo Nordisk itashuka kutoka zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi hadi dola 199, huku Wegovy ya Eli Lilly ikipungua kutoka takribani dola 1,300 hadi dola 199.

Hata hivyo, bei hizo zitapanda taratibu baada ya kipindi cha awali cha miezi miwili, kulingana na maelezo yaliyotolewa kwenye tovuti. Trump alisisitiza kuwa kwa muda mrefu Wamarekani wamekuwa wakilipa bei za juu zaidi duniani, akidai kuwa walikuwa wakisubsidia gharama za dawa katika nchi nyingine.

CHANZO: TRT Afrika