Afrika

Uturuki inasisitiza kuwa ushirikiano na Somalia ni wa kunufaisha pande zote

Uhusiano wa Uturuki na Somalia umekuwa ukiongezeka katika miaka ya hivi karibuni, huku nchi hizo mbili zikitarajiwa kuanza uchimbaji wa mafuta katika pwani ya Somalia mwezi Aprili.

Newstimehub

Newstimehub

20 Februari, 2026

a0c115bade17fde63caeca2acf8e39f29e427813f6993d257e8e4c5cdde9e628

Uturuki imeisisitiza tena dhamira yake ya kuendeleza ushirikiano wenye manufaa ya pande zote na Somalia, huku ikikanusha madai kwamba makubaliano yake ya nishati na Mogadishu yanalenga kunufaisha upande mmoja tu.

“Madai yanayosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii yanayojaribu kuionyesha Uturuki kama nchi inayotafuta faida za upande mmoja katika sekta ya nishati nchini Somalia—hasa kuhusu utafutaji wa mafuta—ni upotoshaji wa makusudi na taarifa zisizo za kweli zinazolenga kudhoofisha ushirikiano wa manufaa ya pamoja kati ya nchi hizo mbili,” Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki ilisema katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi.

Haya yanajiri wakati meli ya Kituruki ya uchimbaji Çağrı Bey, ikielekea Somalia kwa ajili ya uzalishaji wa kwanza kabisa wa mafuta katika historia ya taifa hilo la Pembe ya Afrika—hatua ambayo imeelezwa na pande zote mbili kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wao.

Waziri wa Petroli wa Somalia, Dahir Shire, alisema katika mahojiano na TRT Afrika kuwa uchimbaji huo wa mafuta “uliosubiriwa kwa muda mrefu na wa kihistoria kwa watu wa Somalia.”

‘Nchi ndugu’

Uchimbaji huo wa mafuta, unaotarajiwa kuanza katika pwani ya Somalia mwezi Aprili, unafuatia shughuli za utafiti zilizofanywa mwaka jana na meli ya Kituruki ya Oruç Reis, baada ya nchi hizo mbili kusaini makubaliano katika sekta ya mafuta na gesi kama sehemu ya kuimarisha ushirikiano wao katika sekta mbalimbali.

Taarifa hiyo pia iliongeza kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Shirika la Mafuta la Uturuki (TPAO) na Mamlaka ya Petroli ya Somalia yanaeleza wazi kwamba rasilimali asilia ni mali halali ya watu wa Somalia.

“Uturuki na Somalia zinadumisha uhusiano wao kupitia msingi wa ushirikiano wa pande zote, unaoakisi uhusiano kati ya mataifa mawili huru, yenye urafiki na kindugu,” Uturuki ilisema.

“Wakati mshikamano huu unaendelea kuimarika katika nyanja mbalimbali, ni muhimu kuepuka kutoa taariafa zaupotoshaji na propaganda iliyoundwa kudhoofisha ushirikiano huu,” iliongeza.