Serikali ya Afrika Kusini imegundua zaidi ya wafanyakazi hewa 4,000 kupitia ukaguzi wa mfumo wa mishahara wa PERSAL. Mamlaka zinasema baadhi ya mishahara ililipwa kwa watu waliokufa au kutumia vitambulisho bandia.
Zoezi la uhakiki linaendelea nchi nzima, huku waliokosa kujitokeza wakikabiliwa na kusimamishwa mishahara na hatua za kinidhamu. Serikali inalenga kuokoa mabilioni ya randi na kuboresha uwazi katika matumizi ya fedha za umma.
Chanzo: TRT Afrika














