Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kuwahamisha wanafunzi 43 waliokuwa wakisoma katika vyuo mbalimbali nchini Iran kufuatia kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Wanafunzi hao walitolewa kutoka Tehran kwa usafiri wa barabara hadi mpaka wa Iran na Uturuki, ambapo walipokelewa na maafisa wa ubalozi wa Uganda kabla ya kupelekwa Istanbul kwa usalama zaidi.
Chanzo:TRT Afrika














