Wachezaji saba wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Iran wamepewa hifadhi ya kisiasa nchini Australia kufuatia tukio la kugoma kuimba wimbo wa taifa wakati wa mashindano ya Kombe la Asia yaliyofanyika nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Australia Tony Burke, mmoja wa wachezaji hao alibadili uamuzi wake na kuomba kurudi Iran.
Waziri huyo alisema mchezaji huyo aliwasiliana na maafisa wa ubalozi wa Iran ambao walifika hotelini walikokuwa wamefikia wachezaji hao na kumchukua.
Hata hivyo, wachezaji wengine waliamua kubaki Australia kwa hofu ya usalama wao ikiwa wangerejea Iran.
CHANZO: TRT Afrika














