Kulingana na Iyombe, kufikia sasa, ni kaya 1,678 pekee zilizoondoka ndani ya NCA, kati ya kaya 23,000.Mwenyekiti wa Tume iliyopewa jukumu la kutathmini utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kwa Wakazi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kwenda Msomera mkoani Tanga na maeneo mengine, Mussa Iyombe, amesema zoezi hilo halijafanikiwa kama ilivyotarajiwa.
“Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwa dhamira ya serikali ya kutekeleza zoezi la uhamaji wa hiari ili kuboresha maisha ya wananchi na kulinda ikolojia ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Iyombe wakati akikabidhi ripoti ya tume hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Machi 12, 2026.
Chanzo: TRT Afrika














