Mamii ya raia wa Libya walikusanyika Jumapili kuomboleza kifo cha mkuu wa majeshi, Jenerali Mohammad Ali Ahmad al-Haddad, pamoja na watu wengine saba waliopoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea nchini Uturuki.
Ibada ya mazishi ilifanyika mjini Misrata, alikozaliwa marehemu, na ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibah pamoja na viongozi wa juu wa kijeshi na kisiasa. Baada ya ibada hiyo, miili ilikabidhiwa kwa familia kwa mazishi ya faragha.
Shughuli nyingine za kuomboleza zilifanyika awali mjini Ankara na Tripoli.
Ajali hiyo ilihusisha ndege binafsi iliyokuwa imebeba maafisa wa kijeshi na wahudumu wa ndege, iliyoanguka muda mfupi baada ya kuondoka Ankara. Maafisa wamesema hitilafu ya kiufundi inahisiwa kuwa chanzo, huku uchunguzi ukiendelea kwa kushirikiana na Uturuki.
CHANZO: TRT Afrika














