Rais wa Madagascar, Michael Randrianirina, ametangaza uteuzi wa Mamitiana Rajaonarison kama Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo. Uteuzi huo umefanyika siku chache baada ya rais kuvunja serikali na kumfuta aliyekuwa waziri mkuu.
Rajaonarison alikuwa akiongoza kitengo cha taifa cha ujasusi wa kifedha kinachopambana na utakatishaji fedha na uhalifu wa kifedha tangu mwaka 2021.
Rais amesema anatarajia serikali mpya kuleta mageuzi na kurejesha matumaini ya wananchi katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kisiasa nchini Madagascar.
Chanzo: TRT Afrika














