Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameanza ziara rasmi nchini Uingereza baada ya kuondoka Abuja kuelekea London Machi 17, akiwa ameandamana na mkewe Oluremi na ujumbe wa serikali.
Katika ziara hiyo, atapokelewa na King Charles III pamoja na Queen Camilla katika kasri la Windsor.
Tinubu pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Keir Starmer, ambapo mikataba ya biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiutamaduni inatarajiwa kusainiwa.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, ambao tayari umefikia mabilioni ya pauni kila mwaka.
CHANZO: TRT Afrika














