Sekta ya maua nchini Kenya imeanza kupata hasara kubwa kufuatia athari za vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati. Wakulima wanasema kupungua kwa mahitaji ya bidhaa pamoja na changamoto za usafirishaji kumesababisha hasara ya hadi dola milioni 1.4 kwa wiki.
Kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita, hasara imefikia zaidi ya dola milioni 4.2, huku gharama za usafirishaji zikiongezeka maradufu na safari za ndege kupungua, hali inayosababisha mauzo kushuka kwa kiasi kikubwa.
CHANZO: TRT Afrika














