Rais wa Republic of Congo, Denis Sassou Nguesso, amemteua tena Anatole Collinet Makosso kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Uteuzi huo unafuatia kujiuzulu kwa Makosso na baraza lake la mawaziri, hatua ambayo ni sehemu ya utaratibu wa kikatiba baada ya rais kuapishwa kwa muhula mpya.
Makosso anatarajiwa kuwasilisha orodha mpya ya mawaziri kwa rais hivi karibuni ili kuunda serikali mpya.
Hatua hii imekuja siku chache baada ya Nguesso kuapishwa tena kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa Machi 15.














