Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema alichukua uamuzi wa kufunga njia ambayo ingeiruhusu Iran kupata mapato makubwa ya mafuta, akisema hatua hiyo ni ya kimkakati.
Trump alisema baadhi ya washauri wake walipendekeza kufunguliwa kwa njia hiyo, jambo ambalo lingewezesha Iran kupata hadi dola milioni 500 kwa siku. Hata hivyo, alikataa akisema hataki hilo litokee kabla ya mzozo uliopo kutatuliwa.
Alisisitiza kuwa lengo lake kuu ni kuzuia Iran kupata uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia, ambazo alidai zinaweza kuwa tishio kwa Marekani na eneo la Mashariki ya Kati.
Hatua hiyo imeongeza mvutano katika siasa za kimataifa huku vita ikiendelea kuathiri uchumi wa dunia.














