Iran bado haijatoa maamuzi ya mwisho kuhusu ushiriki wake katika fainali za Kombe la Dunia 2026, kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Iran amesema kuwa serikali ndiyo itakayotoa uamuzi wa mwisho, huku akithibitisha kuwa timu ya taifa inaendelea na maandalizi yake ya mwisho kuelekea mashindano hayo makubwa.
Msemaji wa serikali ya Iran, Fatemeh Mohajerani, alisema kuwa nchi hiyo iko tayari kushiriki, jambo linaloashiria uwezekano mkubwa wa ushiriki licha ya sintofahamu iliyopo.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alikanusha taarifa za kuwepo kwa zuio la wachezaji wa Iran kuingia Marekani, ingawa alisisitiza kuwa baadhi ya watu binafsi wanaweza kuzuiwa.
Kwa upande wake, Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema kuwa Iran inatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo.














