Michezo

Nyota wa zamani wa Nigeria Michael Eneramo afariki baada ya kuanguka uwanjani

Shirikisho la Soka Nigeria lathibitisha kifo chake kufuatia tukio la ghafla wakati wa mechi ya kirafiki.

Newstimehub

Newstimehub

25 Aprili, 2026

686

Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Michael Eneramo, amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa Ijumaa katika eneo la Ungwan Yelwa, Kaduna.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), taarifa za awali zinaonyesha kuwa Eneramo, mwenye umri wa miaka 40, huenda alipata mshtuko wa moyo dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo huo.

Eneramo alikuwa amecheza kipindi chote cha kwanza kabla ya tukio hilo la kushtua kutokea. Katibu Mkuu wa NFF Mohammed Sanusi alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia ya soka ya Nigeria.

CHANZO: TRT Afrika