Kiungo wa timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, amesema anatamani yeye pamoja na wachezaji wenzake waweze kumaliza safari ya kimataifa ya Cristiano Ronaldo kwa kumkabidhi taji la Kombe la Dunia 2026.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa na BBC, Fernandes alisema kuwa itakuwa jambo la kipekee kwa Ronaldo kumaliza Kombe lake la Dunia la mwisho kwa ushindi.
Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, anatarajiwa kushiriki Kombe la Dunia lake la sita mwezi Juni, hatua ambayo itamweka kwenye rekodi ya kipekee katika historia ya mashindano hayo.
CHANZO: TRT Afrika














