Nchini Chad, wananchi wanaanza kutumia mkaa mbadala wa mazingira kama njia ya kupata nishati safi na nafuu.
Mkaa huo hutengenezwa kwa kutumia mabaki ya mimea na taka za kilimo kama maganda ya nafaka, badala ya kutumia miti kama ilivyo kwa mkaa wa kawaida.
Tofauti na mkaa wa kawaida, mkaa huu hutoa moshi mdogo na hivyo kupunguza uchafuzi wa hewa na madhara kwa afya ya binadamu.
Aidha, gharama yake ni nafuu zaidi, jambo linalosaidia familia nyingi zenye kipato cha chini kuupata kwa urahisi.
Wataalamu wanasema matumizi ya mkaa huu yanaweza kupunguza ukataji miti na kusaidia kulinda mazingira kwa muda mrefu.
Serikali na mashirika mbalimbali yanaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati hii ili kuboresha maisha ya wananchi.
Chanzo:BBC News














