Ndege iliyombeba Rais wa Israel Isaac Herzog kuelekea Kazakhstan imelazimika kuchukua njia ndefu ya takribani saa nane baada ya kuepuka kutumia anga ya Uturuki, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.
Kwa mujibu wa Channel 12 ya Israel, ndege hiyo ilipitia Ulaya na Urusi badala ya kutumia njia ya kawaida kupitia anga ya Uturuki, hali iliyoongeza muda wa safari hiyo kwa kiasi kikubwa.
Herzog alithibitisha kupitia mtandao wa X kwamba amewasili salama mjini Astana kwa ziara ya siku mbili nchini Kazakhstan.
Mabadiliko hayo ya njia yanakuja huku mvutano wa kidiplomasia kati ya Israel na Uturuki ukiendelea kuongezeka.














