Serikali ya Afrika Kusini imeondoa rasimu ya kwanza ya sera yake ya taifa kuhusu akili bandia (AI) baada ya kubainika kuwa ilikuwa na marejeo ya vyanzo visivyo halisi katika orodha yake ya rejea.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia za Kidijitali, Solly Malatsi, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marejeo hayo huenda yalitengenezwa na mfumo wa AI bila kuthibitishwa na binadamu kabla ya kuingizwa kwenye waraka huo rasmi.
Malatsi alisema kosa hilo halipaswi kutokea na limeathiri uaminifu pamoja na hadhi ya sera hiyo muhimu ya kitaifa.
Rasimu hiyo ilikuwa imewasilishwa mwezi huu kwa maoni ya umma kabla ya kukamilishwa rasmi.














