Kocha maarufu Jose Mourinho ameibuka kama mgombea mkuu wa kuirejea Real Madrid, kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni.
Inaelezwa kuwa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, anaunga mkono kwa nguvu uwezekano wa kumrudisha Mourinho, ambaye aliwahi kuifundisha timu hiyo kati ya mwaka 2010 hadi 2013.
Wakati huo, Mourinho aliisaidia Real Madrid kushinda taji la La Liga na kuweka rekodi kadhaa, jambo lililomfanya aonekane kama mmoja wa makocha walioacha alama kubwa katika klabu hiyo.
Kwa sasa, inaelezwa kuwa nafasi ya ukocha inaweza kuwa wazi mwishoni mwa msimu, hali inayofanya jina la Mourinho kujitokeza tena kama suluhisho la kuirejesha timu katika ushindani wa juu.
Hata hivyo, ndani ya klabu kuna maoni tofauti, ambapo baadhi ya viongozi hawana uhakika kama Mourinho bado anaweza kuleta mafanikio kama zamani.
Chanzo:Fabrizio Romano














