Rais wa Kenya William Samoei Ruto anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku mbili kuanzia Jumatatu tarehe 4 Mei.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Tanzania, ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, biashara na ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Ruto atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda pamoja na maendeleo ya kiuchumi.
CHANZO: TRT Afrika














