Afrika

Jeshi la Sudan lakomboa maeneo zaidi yaliyokuwa chini ya udhibiti wa RSF

Gavana wa Darfur amesema jeshi limeshika udhibiti wa mji na maeneo jirani baada ya operesheni ya kijeshi dhidi ya RSF.

Newstimehub

Newstimehub

26 Julai, 2026

a0c33725 6082 4b04 86fb b1f08cbff841 1785052071903

Gavana wa Darfur Minni Arko Minnawi amesema kuwa jeshi la Sudan na vikosi washirika limeshika udhibiti wa mji wa Bara na maeneo matatu yaliyo karibu katika jimbo la Kaskazini mwa Kordofan kufuatia operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa RSF.

Kupitia taarifa iliyowekwa katika mtandao wa Facebook Jumamosi, Minnawi amesema jeshi, pamoja na vikosi washirika limeshika udhibiti wa eneo la Bara, Umm Garfa, Umm Sayala na Jabra Al-Sheikh.

“Kilichofanikiwa leo sio mwisho wa mapigano, lakini ni mwanzo wa hatua mpya ya mapambano,” amesema.

Minnawi amesema vikosi vimefanya mashambulizi makali yaliysababisha vifo na uharibifu mkubwa wa vifaa kwa RSF wakati wa kile alichokieleza kuwa “operesheni ya kijeshi” iliyoharibu mfumo wa ulinzi wa RSF.

Mapema Jumamosi, vyanzo vya jeshi vimeiambia Anadolu kuwa jeshi la Sudan na washirika wake limeshika udhibiti wa Umm Sayala karibu na Bara baada ya mapambano na RSF, na kusababisha kile walichokitaja kuwa hasara kubwa kwa RSF.

Video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii imeonesha wanajeshi wakitangaza kudhibiti Umm Sayala pamoja na kuharibu magari ya RSF, ingawa Anadolu haikuthibitisha video hiyo.

Jeshi la Sudan na RSF bado hawajatoa taarifa rasmi kuhusu madai hayo.