Jeshi la Nigeria limeapisha majaji wa mahakama ya kijeshi watakaosikiliza kesi dhidi ya wanajeshi 36 wanaotuhumiwa kuhusika katika njama ya mapinduzi iliyodaiwa kuzimwa mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa Makao Makuu ya Ulinzi ya Nigeria, maafisa hao wa jeshi wanakabiliwa na tuhuma za uasi na kupanga njama za kuiondoa serikali iliyopo madarakani.
Serikali ya Nigeria ilikuwa imekanusha mwishoni mwa mwaka jana kuwepo kwa jaribio la mapinduzi kabla ya baadaye kutangaza mwezi Januari kuwa ilikuwa imefanikiwa kuzuia mpango wa kuipindua serikali.
Mamlaka zimesema mwenendo wa kesi hizo utafanyika kwa kuzingatia viwango vya juu vya haki na uwazi.
CHANZO: TRT Afrika














