Afrika

Rigathi Gachagua arudi mahakamani kusikiliza kesi ya kupinga kuondolewa madarakani

Aliyekuwa Naibu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, leo Alhamisi, Mei 7, amerudi katika Mahakama Kuu jijini Nairobi kusikiliza kwa ombi lake la kupinga kuondolewa madarakani.

Newstimehub

Newstimehub

7 Mei, 2026

2025 05 15t122810z 611303276 rc26ieaefafc rtrmadp 3 kenya politics

Katika usikilizwaji wa kwanza wa shauri hilo uliofanyika Aprili 27, Rigathi Gachagua alidai kuwa mchakato wa kumuondoa madarakani uliotekelezwa na Bunge mwezi Oktoba 2024 ulikuwa kinyume cha Katiba, haukufuata taratibu sahihi, na haukufikia kiwango kinachotakiwa cha ushirikishwaji wa umma kama inavyotakiwa kisheria.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha DCP, alikacha ombi lake la kurudishiwa wadhifa wake, badala yake, akaiomba mahakama hiyo, alipwe fidia na stahiki zake kadhaa, na kutaka kutangazwa kuwa, mchakato wa kumuondoa madarakani ulikiuka Katiba na taratibu za kisheria.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu, ambao wanatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu maombi kadhaa yaliyowasilishwa na pia kusikiliza hoja za msingi za kesi hiyo.

Gachagua anakuwa Makamu wa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondolewa madarakani.