Afrika

Tanzania, Misri ruksa raia wake kuingia Sudan Kusini bila viza

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mpya, ni nchi mbili pekee ambazo zimeongezwa katika orodha ya raia wake kuruhusiwa kuingia bila viza nchini Sudan Kusini, nazo ni Misri na Tanzania.

Newstimehub

Newstimehub

19 Julai, 2026

6c0bf780 036a 4674 8eee 9f83d12b6bdc 1784448831569

Serikali ya Sudan Kusini imetoa orodha mpya ya sera za viza ambapo imeiorodhesha Tanzania na Misri miongoni mwa nchi ambazo raia wake wanaruhusiwa kuingia bila viza au kulipia viza.

Muongozo huo mpya unatoa taarifa zaidi ya vigezo vinavyohitajika kwa wasafiri kutoka mataifa ya Afrika na sehemu nyengine ya dunia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mpya, ni nchi mbili pekee ambazo zimeongezwa katika orodha ya raia wake kuruhusiwa kuingia bila viza nchini Sudan Kusini, nazo ni Misri na Tanzania.

Hata hivyo, raia kutoka mataifa mengine ya Afrika, ikiwemo Ghana na Nigeria hawapo katika orodha hiyo.

Tanzania na Misri, zinaungana na Kenya ambayo pia raia wake wenye hati sahihi ya kusafiria, wanaruhusiwa kuingia nchini Sudan Kusini bila viza wala malipo ya viza. Utaratibu huo ulianza Julai 28, 2021.