Ulimwengu

Trump ataka Infantino awe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Infantino, mwenye umri wa miaka 56, amejenga ukaribu na Rais Trump, hususani wakati wa fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2026, zilizoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada.

Newstimehub

Newstimehub

22 Julai, 2026

328b7359 678a 4704 8fdc 15a9ce44cd22 1784737116302

Rais Donald Trump wa Marekani amempigia chapuo rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino kuwa Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa.

Likikinukuu chanzo cha karibu cha Rais Trump, jarida la the New York Post, lilisema kuwa Trump anaamini kuwa Infantino ana heshima na ushawishi mkubwa duniani, jambo linalodhihirisha uwezo wake wa kuwaleta watu pamoja.

Infantino, mwenye umri wa miaka 56, amejenga ukaribu na Rais Trump, hususani wakati wa fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2026, zilizoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Mexico na Canada.

Kwa sasa, nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inashikiliwa na Antonio Guterres kutoka Ureno, ambaye atamaliza muda wake wa uongozi, Disemba 31, 2026.

Mrithi wa Guterres ndani ya Umoja wa Mataifa anatagemewa kuchukua wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia Januari 1, 2027.