Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema dunia inaingia katika kipindi kipya cha mabadiliko makubwa ya ajira kutokana na kasi ya maendeleo ya akili bandia (AI), roboti na teknolojia za kisasa.
Akizungumza katika Mkutano wa 6 wa Ujuzi wa OECD uliofanyika Istanbul, Erdogan alisema mabadiliko hayo yanafanana kwa ukubwa na yale ya Mapinduzi ya Viwanda yaliyobadili mfumo wa uzalishaji duniani karne zilizopita.
Alisema viwanda vinavyojiendesha vyenyewe kikamilifu, vinavyojulikana kama “dark factories”, vinaonesha wazi namna teknolojia inavyobadilisha ajira za binadamu kwa kasi kubwa.
Kwa mujibu wa Erdogan, serikali duniani zinapaswa kuelewa mabadiliko hayo mapema ili kujiandaa kwa kupotea kwa baadhi ya kazi huku taaluma mpya zikiibuka.
Aliongeza kuwa mtaji wa rasilimali watu utakuwa kipimo kikuu cha nguvu ya taifa katika siku zijazo.














