Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema watoto hawapaswi kamwe kubeba mzigo wa vita, migogoro na umaskini, akisisitiza kuwa kuishi kwa amani ni haki yao ya msingi.
Akizungumza katika tamasha la watoto la kimataifa la TRT lililofanyika mjini Ankara, Erdogan alisema kuwa licha ya juhudi za kidiplomasia, watoto wengi bado wanaendelea kuteseka kutokana na vita na dhuluma.
Aliongeza kuwa Uturuki inaendelea kufanya kazi kuhakikisha migogoro inakoma na watoto wanalindwa dhidi ya madhara ya vurugu.
Kauli hiyo ilitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Uhuru na Watoto ya Aprili 23.
CHANZO: TRT Afrika














