Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar wamefanya mazungumzo ya simu kujadili mwenendo wa mazungumzo yanayoendelea kati ya Marekani na Iran, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza mvutano wa kikanda.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, viongozi hao wawili walijikita zaidi katika hatua za kidiplomasia zinazoweza kuchukuliwa siku zijazo ili kuzuia kuongezeka kwa mgogoro huo. Mazungumzo hayo pia yaligusia nafasi ya Pakistan kama mpatanishi muhimu katika mazungumzo hayo.
CHANZO: TRT Afrika














