Kamanda wa vikosi vya drone vya Ukraine amesema kuwa mkakati wao mpya unalenga kushambulia miundombinu ya mafuta, wanajeshi, na hali ya kisaikolojia ya majeshi ya Russia.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mashambulizi ya drone yamekuwa chombo muhimu katika vita vinavyoendelea, yakitumika kulenga vituo vya mafuta, maghala ya silaha, na njia za usambazaji.
Ameeleza kuwa kulenga sekta ya nishati, hasa mafuta, kunaweza kudhoofisha uwezo wa Urusi kuendesha operesheni zake za kijeshi kwa ufanisi.
Mbali na uharibifu wa vifaa, mashambulizi hayo pia yanalenga kushusha morali ya wanajeshi wa Urusi, kwa kuwa yanazidi kuonyesha udhaifu katika ulinzi wao.
Ripoti zinaonyesha kuwa Ukraine imeongeza uzalishaji wa drone na kuboresha teknolojia yake ili kufikia malengo ya mbali zaidi ndani ya eneo la Urusi.
Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema mkakati huo unaweza kubadilisha mwelekeo wa vita, hasa kwa kuathiri rasilimali muhimu za Urusi.
Chanz:BBC













