Ulimwengu

Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani

Mwanasiasa huyo, aliituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kumtumia kama chambo, kuhalalisha usalama wa kitaifa.

Newstimehub

Newstimehub

20 Oktoba, 2026

04cd89a4 42e5 4c4c 80d8 686fffcd0b7f 1792499220061

Makamu Rais wa Ufilipino, Sara Duterte amedai kuwa, upande wa waendesha mashtaka wa nchi hiyo, wameshindwa kutoa ushahidi wenye kuhalalisha kuondolewa kwake madarakani.

“Baada ya Baraza la Wawakilishi kushindwa kuthibithisha pasi shaka kuwa nastahili kung’olewa madarakani,” alisema Duterte, ambaye ni binti wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte.

Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo, aliituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kumtumia kama chambo, kuhalalisha usalama wa kitaifa.

“Wote tu mashuhuda wa namna serikali inavyotumia kila njia kunishusha chini,” alieleza.