Morocco imetangaza hali ya tahadhari katika mikoa tisa huku moto ukiendelea kuteketeza misitu kwa wiki moja sasa, na picha satelaiti zikionesha hekta zaidi 4,100 sawa na ekari 10,131 zimeteketewa tangu mwanzo wa mwaka huu.
Licha ya hali hiyo, eneo lililoteketezwa mwaka huu linaonekana kuwa dogo ikilinganishwa na moto uliotokea kati ya 2012 na 2025, kulingana na mfumo wa kufuatilia.
Tahadhari kwa moto
Siku ya Ijumaa, Shirika la Taifa la Morocco kuhusu Maji na Misitu lilitoa tahadhari katika mikoa tisa maeneo ya kaskazini na mashariki mwa nchi, ishara ya hali ya hatari ya moto katika misitu.
Shirika hilo linategemea mfumo wa tahadhari ya mapema kulingana na hali ya hewa na ukubwa wa misitu kutathmini hatari ya moto katika misitu.
Takwimu rasmi zilizotolewa mapema zinaonesha mamlaka zimebaini kuwepo kwa matukio 310 ya moto wa misituni kati ya mwanzo wa mwaka na Julai 20, kuteketeza hekta karibu 1,850 ikiwa ni sawa na ekari 4,571.
Misitu nchini Morocco ni karibu 12% ya maeneo ya nchi hiyo, huku mamlaka zikisema kuwa zimepeleka ndege zisizokuwa rubani pamoja na maafisa wa zimamoto ardhini kwa lengo la kudhibiti moto usisambae zaidi.

















