Wabunge wa Ufaransa wanatarajiwa kujadili mswada muhimu unaolenga kurahisisha urejeshaji wa kazi za sanaa zilizoibiwa wakati wa ukoloni.
Ufaransa bado inamiliki maelfu ya kazi za sanaa na vitu vya thamani vilivyochukuliwa kutoka nchi mbalimbali, hasa barani Afrika, wakati wa utawala wa kikoloni.
Mswada huo unachukuliwa kama hatua muhimu ya kurekebisha makosa ya kihistoria na kurejesha haki kwa mataifa yaliyoathirika.
CHANZO: TRT Afrika














