Afrika

Spika wa zamani wa Nigeria Tambuwal akamatwa kwa madai ya ufisadi wa milioni $123

Aminu Tambuwal alikamatwa Jumatatu katika mji mkuu, Abuja, kwa madai ya ubadhirigu wa fedha karibu Naira bilioni 189 (milioni $123).

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

bdf24a3cf207d44144af9225b0df4b64468258b8a710ff182894ca47d2da9278

Spika wa zamani wa bunge la Nigeria ambaye baadaye alikuwa gavana wa jimbo la Sokoto amekamatwa na Tume ya kupambana na ufisadi wa Kiuchumi na Fedha (EFCC) kuhusu madai ya ufisadi

Aminu Tambuwal alikamatwa Jumatatu katika makao makuu ya tume jijini, Abuja, kuhusiana na ubadhirifu wa fedha karibu Naira bilioni 189 (milioni $123).

Haifahamiki kama nafasi zake za zamani zina uhusiano wowote na madai hayo. Tambuwal mwenye umri wa miaka 59 alikuwa bado anahojiwa Jumatatu jioni na hajazungumzi wazi kuhusu madai hayo.

Madai ya kutoa pesa hizo yanaaminika ni ukiukwaji wa sheria ya Kutakatisha Fedha ya 2022, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti.