Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na maafisa wakuu wa makampuni ya gesi na mafuta katika Ikulu ya White House kujadili athari za vita dhidi ya Iran kwenye sekta ya nishati.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, kikao hicho kilijikita katika hatua za kuchukua iwapo Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa kwa muda mrefu, pamoja na athari zake kwa soko la kimataifa la mafuta.
Miongoni mwa waliohudhuria ni Waziri wa Nishati Scott Bessent, Makamu wa Rais JD Vance pamoja na maafisa wengine waandamizi wa utawala wa Marekani.
Mazungumzo hayo pia yalihusu uzalishaji wa ndani wa mafuta, usafirishaji wa nishati na hali ya sekta ya mafuta Venezuela.
CHANZO: TRT Afrika














