Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Greenland ni muhimu sana kwa maslahi ya kiusalama na kwamba Marekani “lazima iichukue.” Akizungumza kabla ya Jukwaa la Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump alidai Denmark haina uwezo wa kuilinda ipasavyo, akisisitiza kuwa suala hilo litajadiliwa na viongozi wa dunia wanaohudhuria mkutano huo.
Trump alieleza kuwa NATO imekuwa ikionya Denmark kwa zaidi ya miongo miwili kuhusu vitisho vya kiusalama katika eneo la Arctic, akitaja Urusi na China kama changamoto kubwa. Licha ya kuisifu Denmark na uongozi wake, alisisitiza kuwa Marekani italazimika kuchukua hatua.
CHANZO: TRT Afrika














