Bobi Wine amemtaka Rais Yoweri Museveni kuepuka matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi, akisisitiza kuwa wito wake ni wa maandamano ya amani yanayolindwa na Katiba. Alidai serikali inadhibiti kampeni za upinzani, ikiwemo kufunga vituo vya redio na kukamata wafanyakazi wake. Rais Museveni, mgombea wa urais wa 2026, amekanusha madai hayo na kuonya dhidi ya vurugu, huku akisisitiza kuwa serikali iko tayari kulinda usalama wa nchi.
CHANZO: BBC NEWS














