Uchumi Maisha Ulimwengu

Vita ya Iran Yatishia Mabilioni ya Milo Duniani.

Mkuu wa kampuni kubwa ya mbolea ameonya kuwa vita inayohusisha Iran inaweza kuhatarisha uzalishaji wa chakula duniani.

Newstimehub

Newstimehub

1 Mei, 2026

452587b0 4525 11f1 bd52 e755d604ece4.jpg

Mgogoro wa vita unaoihusisha Iran umeanza kuleta athari kubwa katika sekta ya kilimo duniani, huku mabilioni ya milo yakihofıwa kupotea kutokana na upungufu wa mbolea,mkurugenzi mkuu wa kampuni kubwa ya mbolea duniani, Yara, amesema kuwa hadi milo bilioni 10 kwa wiki inaweza kuwa hatarini kutokana na upungufu wa mbolea unaosababishwa na vita hiyo.

Sababu kubwa ya hali hiyo ni kuzuiwa kwa usafırishaji kupitia Mlango wa Hormuz, njia muhimu inayotumika kusafırisha mbolea na malighafı zake. Hali hiyo imesababisha uzalishaji wa mbolea kupungua na bei kupanda kwa kasi.

Wataalamu wanaonya kuwa wakulima wakikosa mbolea ya kutosha, mavuno yanaweza kushuka hadi asilimia 50 kwa baadhi ya mazao, hali itakayopunguza uzalishaji wa chakula duniani.

Nchi maskini ndizo zinazotarajiwa kuathirika zaidi kwani hazina uwezo wa kushindana kununua chakula au mbolea kwa bei ya juu, Hali hiyo inaweza kusababisha njaa na uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo mengi ya dunia.

Chanzo:BBC World