Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kuachana na nia ya kujiunga na NATO ikiwa nchi yake itapatiwa dhamana za usalama zitakazohakikisha ulinzi wa muda mrefu. Kauli hiyo imetolewa wakati mazungumzo ya kidiplomasia yanayoongozwa na Marekani yakiendelea, yakilenga kumaliza vita kati ya Ukraine na Urusi. Hata hivyo, Kyiv imeonyesha wasiwasi kuhusu mapendekezo ya Marekani yanayohusisha kuondoa wanajeshi mashariki mwa nchi, ikisisitiza kuwa haitakubali kutoa ardhi wala mpango wowote unaoweza kuhatarisha usalama wake wa baadaye.
CHANZO: BBC NEWS














