Afrika

CHAN 2024: VAR ‘yaokoa milioni moja’ ya Rais William Ruto

Hii ni baada ya timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ kutoka suluhu na timu ya taifa ya Angola, katika mchezo wao wa pili wa Kundi A, uliofanyika Agosti 7, 2025.

Newstimehub

Newstimehub

7 Agosti, 2025

4f9d1101c086063c778fb15bdd125f7331aa0a19a50ceb5d711260e0ca6f6fd5

Wachezaji na benchi la ufundi la timu ya taifa ya Kenya, ‘Harambee Stars’ watalazimika kuweka kibindoni Shilingi 500,000 tu za Kenya, na sio kitita cha Shilingi 1,000,000 kama walivyoahidiwa na Rais William Ruto, baada ya kutoshana nguvu na Angola, katika mchezo wa pili wa Kundi A wa michuano ya CHAN 2024, uliofanyika Agosti 7, 2025 katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Angola, maarufu kama ‘Paa Weusi’ ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani, kupitia bao la dakika ya 7 ya mchezo, lililowekwa kimiani na Jó Paciência.

Hata hivyo, ‘Harambee Stars’ walicharuka na kusawazisha dakika tano baadaye, kupitia kwa nyota wao, Austin Odhiambo.

07cefdf2942f045e88f417cc1fb322365ad70257c4fd1bdad0a4221005677d8c 1

Kenya ilipata pigo katika dakika ya 21 ya mchezo baada ya Marvin Omondi kuoneshwa kadi nyekudu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Angola, na hivyo kulazimika kucheza pungufu hadi mwisho wa mchezo.