Tangu kuingia ofisini mwezi Januari, utawala huo haujaeleza hadharani msimamo kuhusu mpango huo wa kibiashara, unaojulikana kama AGOA, sheria iliyopitishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 ili kutoa ufikiaji bila ushuru katika soko la Marekani kwa maelfu ya bidhaa.
Licha ya uungwaji mkono mpana wa pande mbili za kuunda upya AGOA, huku wanaounga mkono wakisema inasaidia kubadilisha minyororo ya ugavi ya Marekani na kukabiliana na ushawishi wa China barani Afrika, matarajio ya mpango huo kuongezwa kabla ya kuisha hayana uhakika.
Njia yake pekee ya kisheria ni kuambatanishwa na mswada wa ufadhili wa Marekani ambao Chama cha Republican kinashinikiza ili serikali ya Marekani kutofungwa baada ya siku ya Jumanne 1 Oktoba, ingawa inaweza kuongezwa muda waka hata baadaye.
Serikali za Kiafrika na wawekezaji wamekuwa wakishawishi katika wiki za hivi karibuni kutaka kuongezwa kwa mwaka mmoja au miwili baada ya juhudi za kupata kuogezwa kwa muda mrefu kutoweza kupita katika Bunge la Congress.
AGOA ina sifa ya kusaidia mamia ya maelfu ya kazi katika zaidi ya nchi 30.
Athari zake zimepunguzwa na michakato ya ushuru ambao Trump alianzisha mwezi Agosti. Hapo awali chini ya mpango wa AGOA bidhaa ziliuziwa Marekani bila ushuru.














