Afrika

Jumba kuu la makumbusho Libya lafuguliwa kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa Gaddafi

“Kufunguliwa tena kwa Makumbusho ya Taifa si tukio la kitamaduni tu, bali ni ushahidi kwamba Libya inajenga upya taasisi zake,”
— Abdulhamid al-Dbiebah, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Newstimehub

Newstimehub

14 Desemba, 2025

1765639084743 5d1phb 8f156f9a1514894b2e8cea7d5a9e7f02524bad8a8be56a174125bdb7d0c3cd83

Makumbusho ya Taifa ya Libya, yanayojulikana kama Red Castle, yamefunguliwa tena mjini Tripoli kwa mara ya kwanza tangu yalipofungwa mwaka 2011 kufuatia kuangushwa kwa Muammar Gaddafi. Makumbusho hayo, makubwa zaidi nchini humo, yanaonyesha hazina za kihistoria kuanzia enzi za kabla ya historia hadi nyakati za Kirumi, Kigiriki na Kiislamu, huku serikali ikisema ufunguzi huo ni hatua muhimu katika kurejesha urithi wa kitamaduni na kuimarisha taasisi za taifa.

CHANZO: TRT Afrika