Mkuu wa majeshi ya Sudan Abdel Fattah al-Burhan amesema yuko tayari kushirikiana na Rais wa Marekani Donald Trump katika juhudi za kumaliza mgogoro wa Sudan. Kauli hiyo ilitolewa baada ya ziara yake Saudi Arabia, huku juhudi za amani zikiendelea kukwama kutokana na tofauti kati ya Sudan na wapatanishi wa kimataifa.
CHANZO: TRT Afrika














